Canada kuondosha vikosi vyake Afghanistan | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.11.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Canada kuondosha vikosi vyake Afghanistan

Canada imesema itawarejesha nyumbani wanajeshi wake, kutoka Afghanistan.

default

Waziri mkuu wa Canada, Stephen Harper.

Canada inajitayarisha kuviondoa vikosi vyake kutoka Afghanistan. Kuambatana na uamuzi uliopitishwa na bunge la nchi hiyo,wanajeshi wake watakuwa wamerejea nyumbani ifikapo mwisho wa mwaka 2011. Msemaji wa kijeshi amesema, mkuu wa majeshi ametoa amri ya kuanza kuwarejesha nyumbani wanajeshi 2,800 walioko kusini ya Afghanistan.

Waziri Mkuu wa Kanada Stephen Harper ameeleza waziwazi kuwa yeye hatorefusha muda wa vikosi vyake nchini Afghanistan hata akiombwa na Rais wa Marekani Barack Obama.Tangu mwaka 2002, Kanada imepoteza wanajeshi 133 na mwanadiplomasia mmoja nchini Afghanistan.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com