Bush na Olimpik | Michezo | DW | 07.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bush na Olimpik

Rais Bush aishambulia china masaa 24 kabla ufunguzi wa olimpik.

Bush na Hu Jintao

Bush na Hu Jintao

China ikijiandaa kwa ufunguzi rasmi hapo kesho wa michezo ya 29 ya Olimpik ya kisasa na kuitisha pasichanganywe siasa na spoti, mgeni mashuhuri katika ufunguzi wa kesho Rais George Bush wa Marekani, ameelezea wasi wasi mkubwa juu ya tabia ya China ya kuwaweka kizuizini wapinzani na kukiuka kwake kwa haki za binadamu.China yadai Bush aliahidi kutoingiza siasa katika michezo.

►◄

Michezo ya 29 ya olimpik itafunguliwa masaa 24 kutoka sasa na kiasi cha viongozi wa dola na serikali 80 wameanza kuwasili Beijing kuhudhuria sherehe za kesho.Rais George Bush wa Marekani, akiwa nchi jirani ya Thailand akielekea Beijing,alielezea leo wasi wasi mkubwa juu ya hatua za China za kuwatia kizuizini wapinzani na kuwa haiheshimu haki za binadamu.

"Marekani inasimama kidete kupinga tabia ya China ya kuwatia kizuizini wapinzani,wakereketwa wa haki za binadamu na wanotetea uhuru wa kuabudu."

Akizungumza leo mjini Bangkok,Thailand, Rais Bush alisisitiza kuwa ila anazotoa hakusudii kuiudhi China katika mkesha wa ufunguzi rasmi wa michezo.Bush alielezea matumaini mazuri juu ya mustakbala wa taifa hili kuu lenye wakaazi wengi mno duniani.

"Tunatetea uhuru wa vyombo vya habari na watu kujumuika,haki za wafanyikazi tena bila ya kuudhi uongozi wa China.Lakini, kuwapa watu wake uhuru mkubwa zaidi, ndio njia pekee kwa China kuukuza uwezo wake kamili ilionao."

Wakosoaji wa siasa za China kama vile katika mzozo wa Dafur,nchini Sudan na ule wa Tibet, walimtaka rais Bush kususia sherehe za kesho za ufunguzi wa michezo ya Beijing.

China kwa upande wake imesisitiza kuwa michezo mikubwa kabisa ulimwenguni-Olimpik isichanganywe na siasa na ni swali ambalo rais Bush aliahidi kuitikia.

Bingwa wa Marekani wa mchezo wa kukimbia kwa kasi katika barafu

Joey Cheek, mjumbe mashuhuri wa kikundi kinachotetea haki za binadamu kwa Dafur,alifutiwa visa yake ya kuhudhuria michezo ya Olimpik ya Beijing .

Bush ametetea uamuzi wake wa kuhudhuria michezo hii ya Olimpik akidai atawashangiria wanariadha wa kimarekani huku akionesha heshima zake kwa China.

huku Beijing ikijiandaa kwa ufunguzi rasmi wa kesho na kukuza heba yake kama dola kuu ulimwenguni kupitia medani ya olimpik,rais Bush amekuwa akiishinikiza China kujitwika jukumu kubwa zaidi katika maswali ya kilimwengu.

Katika medani ya michezo halisi ya olimpik, leo ni zamu ya dimba la timu za wanaume-Brazil ikiwa na miadi na Ubelgiji,Argentina na Ivory Coast .