JangaAfrika
Burundi yahitaji msaada kukabiliana na mafuriko makubwa
18 Aprili 2024Matangazo
Burundi, ambayo Umoja wa Mataifa unasema ni miongoni mwa nchi 20 zilizo katika hatari kubwa ya kukabiliwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, imekumbwa na mvua isiyo na kikomo tangu mwezi Septemba mwaka jana, huku mji wake mkuu wa Bujumbura ukiharibiwa pakubwa na mafuriko kutokana na ujazo wa ziwa Tanganyika kuongezeka.
Soma pia:Mvua kubwa yasababisha maafa katika mataifa mengi duniani
Eneo la Afrika Mashariki limekuwa likikumbwa na mvua kubwa katika wiki za hivi karibuni ambazo zimegharimu maisha ya takriban watu 58 nchini Tanzania tangu kuanza kwa mwezi huu huku wengine 13 wakifariki nchini Kenya.