Brussels. Russia yashutumiwa kwa polisi wake kuwapiga waandamanaji. | Habari za Ulimwengu | DW | 17.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Brussels. Russia yashutumiwa kwa polisi wake kuwapiga waandamanaji.

Umoja wa Ulaya , Ujerumani na Marekani zimeilaumu Russia kuhusiana na polisi kuwapiga na kuwatawanya waandamanaji wanaoipinga serikali mjini Moscow mwishoni mwa juma lililopita.

Serikali ya Russia imetetea hatua hiyo ya polisi, ikisema kuwa waliwalenga watu wenye msimamo mkali.

Umoja wa Ulaya umedai kuwa Russia ilinde haki ya watu kutoa mawazo yao.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema kuwa serikali yake inatarajia ufanyike uchunguzi wa kina kuhusiana na hatua hiyo ya polisi, ikiwa ni pamoja na kuwakamata waandishi wa habari wa televisheni ya taifa ya Ujerumani mjini Moscow.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com