1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brexit haitaiathiri Ligi ya Premier ya England

24 Juni 2016

Uamuzi wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya hautuaiathiri ufarahari wa ligi maarufu kabisa ya kandanda ulimwenguni, Premier League ya England. Hayo ni mwa mujibu wa msemaji wa ligi hiyo

https://p.dw.com/p/1JCbE
Leicester City Spieler
Picha: picture-alliance/dpa/J. Super

Mwaka jana, wachezaji 432 wa Ulaya walisajiliwa kucheza katika Premier League ambayo ina timu 20 – ambapo baadhi ya majina makubwa barani Ulaya yanapatikana katika vilabu vikubwa vya England.

Ijapokuwa hapatakuwa na athari za maramoja kwa wachezaji wa Umoja wa Ulaya ambao tayari wako katika Premier League, huko mbeleni huenda ikawa vigumu kwa vilabu vya England kuwasaini wachezaji wapya.

Hata hivyo msemaji wa ligi hiyo maarufu amesema bado ni mapema mno kutoa utabiri kuhusu athari zitakazotokana na kura ya Brexit. Kwa sasa, wachezaji kutoka nje ya Umoja wa Ulaya wanastahili kutimiza masharti fulani kabla ya kupewa vibali vya kazi kama vile wawe wamecheza asilimia 30 ya michuano ya vilabu vyao vya awali kwa miaka miwili kabla ya kuhamia England.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu