1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boris Johnson akataa kujiuzulu

Saumu Mwasimba
6 Julai 2022

Waziri mkuu Boris Johnson nchini Uingereza amekataa kujiuzulu licha ya kukabiliwa na shinikizo kubwa la kisiasa ikiwemo kutoka ndani ya chama chake,huku baadhi ya watendaji muhimu katika serikali yake wakijiuzulu

https://p.dw.com/p/4DljR
UK Fragen für den Premierministers | Boris Johnson
Picha: REUTERS

Katika kipindi cha saa 24 zilizopita waziri mkuu huyo ameshuhudia akikimbiwa na wimbi kubwa la watendaji wake  serikalini ikiwemo mawaziri wake muhimu.

Ndani ya muda mfupi Boris Johnson amekimbiwa na washirika wake chungunzima serikalini.

Mbele ya bunge leo waziri mkuu Boris Johnson  ameshikilia kwamba hakubaliani na wabunge kutoka chama chake wanaomtaka ajiuuzulu na kuweka mbele maslahi ya taifa.

Boris Johnson anasema haamini ni kinyume na maslahi ya taifa kuendelea kuweko kwake madarakani bali anaamini huu hasa ni wakati ambapo anatakiwa kusimama imara katika kuiongoza nchi.

soma pia: Mawaziri 2 muhimu wajiuzulu Uingereza, shinikizo kwa Johnson

ameliambia bunge kwamba wakati nchi inakabiliwa na shinikizo  kuhusu hali ya kiuchumi,vita vikubwa kabisa ulaya tangu miaka 80 iliyopita ameitaja  huu hasa ndio wakati ambao serikali inatarajiwa  kuendelee kufanya kazi yake kikamilifu.

"Isifunge virago na kuondoka badala yake kuendelea na kazi na kutazama vitu ambavyo vina umuhimu zaidi kwa watu wa nchi hii'' Alisema Boris

Watendaji wake waendelea kujiuzulu

Watendaji wake 13 serikali ikiwemo mawaziri muhimu wa fedha na afya wamejiuzulu, maafisa hao wamejiuzulu wakisema hawezi tena kufanya kazi chini ya uongozi ulioandamwa na kashfa.

Großbritannien Brexit David Frost
wanasiasa David Frost ambae alikuwa karibu na Boris Johnson wakati wa mchakato wa Brexit Picha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Kwa mara nyingine Dadiv Davis mbunge kutoka chama chake cha Conservative ambaye aliwahi kumtaka waziri mkuu huyo ajiuzulu ameliambia bunge leo kwamba kwa mara nyingine anamuomba kiongozi huyo achukue hatua hiyo ya kiungwana ya kujiuzulu kutanguliza mbele maslahi ya nchi kabla ya maslahi yake binafsi.

Hivi sasa unaweza kusema kwamba waziri mkuu huyo wa Uingereza hivi sasa anapambania uhai wake wa kisiasa kufuatia kishindo hiki cha kujiuzulu watendaji wake na kashfa zinazomuandama.

Hata  aliyekuwa mjumbe wake katika mazungumzo ya Brexit David Frost naye pia amejiunga na kundi linalomtaka ajiuzulu  mara moja la chama chake cha wahafidhina.

soma pia:Boris Johnson aponea kura ya kutokuwa na imani naye

Lakini pia wako mawaziri wengine chungunzima waliomtetea waziri mkuu akiwemo naibu waziri mkuu Dominic Raab,waziri wa mambo ya nje Liz Truss na waziri wa mambo ya ndani Priti Patel.

Kujiuzulu kwa watendaji  ni shinikizo lingine kwa Johnson

Mpaka hivi sasa kuendelea kuwa watiifu kwa Johson mawaziri hao kunaondowa uwezekano wa kuitishwa mara moja uchaguzi wa mapema nchini Uingereza.

Ili hicho kitoke ni mpaka atakapokubali Johnson kujiuzulu au kukabiliwa tena na kura ya kutokuwa na imani nae.

Kujiuzlu kwa watendaji muhimu na maafisa wa serikali ya Uingereza kumechochea na hatua ya kuteuliwa mnadhimu wa shughuli za serikali Chris Pincher ambaye wiki iliyopita aliandika barua ya kujiuzulu baada ya kutuhumiwa kulewa na kufanya kitendo cha utovu wa nidhamu dhidi ya wanaume wawili.

Lakini ikidaiwa kwamba sio mara ya kwanza kwa afisa huyo kufanya vitendo vya ukosefu wa nidhamu.