1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Bolsonaro ahukumiwa miaka 27 kwa jaribio la mapinduzi

12 Septemba 2025

Jopo la majaji wa Mahakama ya Juu ya Brazil lilimuhukumu rais wa zamani Jair Bolsonaro kifungo cha miaka 27 na miezi mitatu jela baada ya kumtia hatiani kwa kujaribu kufanya mapinduzi.

https://p.dw.com/p/50NJM
Brazil Brasília 2025 | Jair Bolsonaro
Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro, ambaye sasa amehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa hatia ya kupanga njama ya mapinduzi.Picha: Sergio Lima/AFP

Majai walisema rais huyo wa zamani alikula njama za kusalia madarakani licha ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2022.

Majaji wanne kati ya watano wa mahakama hiyo walisema kwenye hukumu hiyo ya Alhamis (Septemba 111) kwamba walimtia hatiani mwanasiasa huyo wa mrengo mkali wa kulia kwenye mashitaka matano, likiwemo la kupanga njama ya kumuua hasimu wake, rais wa sasa Lula da Silva .

Watuhumiwa wengine kwenye kesi hiyo nao pia walihukumiwa vifungo vya aina mbalimbali, akiwemo waziri wa zamani wa ulinzi, Jenerali Braga Netto, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 26 jela.

Mawakili wa Bolsonaro , ambaye amekuwa akikanusha kutenda kosa lolote, walisema wangeliukatia rufaa uamuzi huo.

Hadi hapo, alikua bado anashikiliwa kwenye kifungo cha nyumbani mjini Brasilia.