1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bodi ya amani ya Trump kuanzisha eneo la ''kibinadamu'' Gaza

8 Julai 2026

Bodi ya Amani ya Rais wa Marekani Donald Trump inapanga kuanzisha eneo la majaribio la "kibinadamu" kusini mwa Ukanda wa Gaza, ambalo linakusudiwa kuwahifadhi maelfu ya raia wa Kipalestina watakaokuwa wamehakikiwa.

https://p.dw.com/p/5Gm3E
Ukanda wa Gaza Maghazi 2026 | shambulizi la Israel
Uharibifu uliosababishwa na shambulizi la Israel katika eneo la Maghazi, Ukanda wa Gaza mnamo Juni 12, 2026Picha: Eyad Baba/AFP

Afisa mmoja ameliambia shirika la habari la AFP kwamba eneo hilo linaweza kuwa "hatua ya kuanzia" kwa kamati ya wataalamu wa Kipalestina, ambayo imekusudiwa kusimamia shughuli za kila siku za utawala wa Gaza katika kipindi cha mpito kutoka vitani, kwa mujibu wa mpango wa vipengele 20 wa Trump.

Eneo hilo la majaribio, ambalo linapangwa kujengwa mjini Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza, litalindwa na vikosi vya kimataifa kutoka kundi la ISF, taasisi mpya inayofanya kazi chini ya Bodi ya Amani.

Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Gaza, ambayo ni kundi la wataalamu wa Kipalestina lililoanzishwa na Bodi hiyo ya Amani, itasimamia zoezi la kuwahakiki watu na kudhibiti uingiaji na utokaji katika eneo hilo, kwa usaidizi wa vikosi vya ISF.