1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayer Leverkusen imeichapa Roma 2-0

3 Mei 2024

Timu ya Bayer Leverkusen imeonesha kuijongelea fainali ya Ligi ya Europa baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Roma katika mchezo wake wa ugenini huko Italia kuendeleza rekodi yao ya kutoshindwa kwa mechi 47 walizocheza.

https://p.dw.com/p/4fSC7
Nusu fainali ya Ligi ya Europa | AS Roma - Bayer Leverkusen
AS Roma na Bayer Leverkusen katika hatua ya nusu fainali ya mchuano wa Ligi ya Europa.Picha: Ciro De Luca/REUTERS

Mabao katika kila nusu ya kipindi cha kwanza cha mnyukano huo kutoka kwa Florian Wirtz na Robert Andrich yaliwahakikishia vijana wa Xabi Alonso ushindi katika mji mkuu wa Italia na kuwapa mabingwa hao wa ligi ya Ujerumani, Bundesliga nafasi kubwa ya kutinga fainali huko Dublin baadaye mwezi huu.

Leverkusen itakutana na Atalanta au Marseille huko Ireland ikiwa watacheza vyema huko Ujerumani wiki ijayo. Kwa uthibitisho wa uchezaji wao huko Roma, watapewa nafasi kubwa ya kushinda taji lao la kwanza kabisa la Europa tangu Kombe la UEFA kuanzishwa kwake.

Leverkusen na unahitaji wake wa ushindi wa mfululizo

Kikosi cha Alonso kilihitaji msururu wa mabao ya dakika za lala salama ili kuendeleza muendelezo wao wa kutoshindwa katika wiki za hivi karibuni lakini pia mchezo wa katika mji mkuu wa Italia ulionesha wazi ubora wa Leverkusen. Roma kwa upande wao wanakabiliwa na kibarua kigumu ikiwa wanataka kutinga fainali ya tatu ya Europer baada ya miaka mingi.

EM 2024-Qualifikation – Gruppe C – Ukraine – Italien
Mchezaji wa Italia Gianluca Scamacca akiruka kwa kichwa wakati wa mechi ya Kundi C ya kufuzu kwa Euro 2024 kati ya Ukraine na Italia Uwanja wa BayArena mjini Leverkusen, Ujerumani, Nov. 20, 2023Picha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance

Katika mnyukano mwingine,Olympique de Marseille wamelazimishwa kutoka sare ya 1-1 nyumbani kwao Ufaransa na Atalanta katika mchezo wao wa mwanzo wa nusu fainali ya Ligi ya Europa.

Mshambuliaji, Gianluca Scamacca na rekodi ya bao la 16

Mshambuliaji, Gianluca Scamacca aliipa timu yake ushindi wa mwanzo kunako  dakika 11 na hivyo kumpa bao lake la 16 katika michuano yote msimu huu. Lakini Chancel Mbemba aliisawazishia Marseille dakika tisa baadae kwa shuti kali la mbali kutinga wavuni kufuatia mpira wa kona.

Pande zote mbili zilikosa nafasi za kufunga mabao zaidi katika kipindi cha pili cha mchuano huo wa aina yake.

Soma zaidi:Bayer Leverkusen wametinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Na kama ilivyelezwa hapo awali, Marseille nayo itasafiri hadi Bergamo kwa mkondo wa pili Alhamisi ijayo. Washindi watakutana na AS Roma au Bayer Leverkusen katika fainali Mei 22 mjini Dublin.

Vyanzo: RTR/AFP