1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayer Leverkusen yatua London kukwaana na West Ham

18 Aprili 2024

Timu ya Bayer Leverkusen iliwasili mjini London, Uingereza, siku ya Alhamisi (Aprili 18) kwa ajili ya kuchuana na West Ham katika mechi ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Ulaya.

https://p.dw.com/p/4ew2c
Bundesliga I Bayer Leverkusen vs Werder Bremen
Wachezaji wa Bayer Leverkusen wakishangiria ushindi dhidi ya Werder Bremen siku ya Jumapili, 14 Aprili 2024.Picha: Martin Meissner/AP/picture alliance

Mabingwa hao wapya wa Bundesliga walitazamiwa kuingia dimbani usiku wa Alhamisi, baada ya kuilaza West Ham 2-0 katika mkondo wa kwanza wa mashindano haya.

Kocha wa Leverkusen, Xabi Alonso, alisema alikuwa na imani kuwa kikosi chake kingelikuwa imara baada ya sherehe za ubingwa ili kuendeleza azma yao ya kusaka mataji matatu msimu huu.

Bayern Munich, Borussia Dortmund kuiwakilisha Ujerumani

Kocha wa West Ham, David Moyes, naye alikuwa na matumaini ya kupindua meza baada ya mchezaji wake, Jarrod Bowen, kurejea mazoezini siku ya Jumatano (Aprili 17).

Wachambuzi wa soka walikuwa wanahofia kuwa baada ya sherehe, Leverkusen inaweza kuwa dhaifu.

Soma zaidi: Bayern Munich yatinga nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya

Katika mechi nyengine, AS Roma ilitarajiwa kushuka dimbani na AC Milan, Marseille itaikaribisha Benfica, huku Livepool ikiwa ugenini Italia na lengo la kupindua matokeo ya 3-0 dhidi ya Atalanta.