1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Ayatollah Khamenei aiomba Iran kurejesha mahusiano na Misri

29 Mei 2023

Kiongozi wa juu zaidi nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema leo kwamba ataikaribisha hatua ya kurejeshwa kikamilifu kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi yake na Misri.

https://p.dw.com/p/4RwNq
Iran Teheran Ayatollah Ali Chamenei
Picha: Iranian Supreme Leader'S Office/Zuma/picture alliance

Kituo cha televisheni cha serikali kimemnukuu Ayatollah Khamenei, baada ya kukutana na Sultan Oman Haitham bin Tariq wa Oman, anayezuru Iran kwa mara ya kwanza tangu alipoingia madarakani mwaka 2020. Muscat kwa muda mrefu imesimama kama mpatanishi katika mvutano kati ya Tehran na Magharibi.

Ishara zinazidi kuwa wazi za kurejea kwa mahusiano baina ya Iran na Misri na hasa baada ya Saudi Arabia na Iran kukubaliana kumaliza mvutano mnamo mwezi Machi chini ya usimamizi wa China. Cairo inaitegemea Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba kuisaidia kiuchumi.

Misri hakikuzungumzia mara moja matamshi hayo ya Khamenei.