AUGUSTA: Jamaa na marafiki wamuaga James Brown
31 Desemba 2006Matangazo
Jamaa, marafiki, mashabiki na viongozi wa haki za raia wamekusanyika kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanamuziki wa miondoko ya soul, James Brown, wiki moja baada ya kifo chake.
Maelfu ya watu wamesafiri kwenda mjini Augusta alikozaliwa mwanamuziki huyo kutoa heshima zao katika sherehe ya hadhara kwenye ukumbi wa James Brown mjini humo. James Brown alifariki dunia siku ya kulalia sikukuu ya Krimasi huko Atlanta akiwa na umri wa miaka 73.