AU yaitisha mazungumzo ya kitaifa ya Walibya mwezi Julai | Matukio ya Kisiasa | DW | 13.03.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

AU yaitisha mazungumzo ya kitaifa ya Walibya mwezi Julai

Mkutano wa kamati maalumu ya umoja wa afrika  kuhusu mzozo wa Libya imeitisha mazungumzo ya kitaifa ya Walibya mwezi Julai mjini Addis-Ababa, Ethiopia.

Mwenye kiti wa kamisheni ya umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat akihutubia kiako cha ufunguzi wa mkutano wa kilele wa marais na viongozi wa serikali za nchi wanachama wa umoja huo.

Mwenye kiti wa kamisheni ya umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat akihutubia kiako cha ufunguzi wa mkutano wa kilele wa marais na viongozi wa serikali za nchi wanachama wa umoja huo.

Mkutano wa kamati maalumu ya umoja wa afrika  kuhusu mzozo wa Libya imeitisha mazungumzo ya kitaifa ya Walibya mwezi Julai mjini Addis-Ababa, Ethiopia. Kamati hiyo inayongozwa na rais wa Congo-Brazzaville Denis Sassou Nguesso ilikutana jana na kuhudhuriwa pia na marais wa Afrika  Kusini na Chad na vilevile mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika. Mkutano huo umekuja katika juhudi za viongozi wa afrika kutatua mzozo wa Libya.

Kwenye taarifa ya pamoja ilisomwa baada ya kumalizika mkutano huo,  waziri wa mambo ya nje wa Congo-Brazzaville, Jean-Claude Ngakosso, alisema viongozi walioshiriki wamepinga uingiliaji kati wa nchi za nje katika mzozo wa Libya na ukiukaji wa marufuku ya silaha kuhusu katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

''Kamati ya kutafuta suluhisho ya mzozo wa Libya imeamua kuitisha mkutano wa kitaifa wa waLibya mwezi julai 2020 kulingana na hatua ya marais wa AU ilichukuliwa mwaka 2018'',inaelezea taarifa hiyo.

 Wakati huohuo kamati hiyo imelaani ''kupelekwa na matumizi ya wapiganaji kutoka nje ya Libya kwenye mzozo unaondelea hivi sasa''ilisema taarifa ya pamoja.

Nyamazisha silaha barani afrika

Mbali na mwenyeji, rais wa Jamhuri ya Congo Denis Sassou Nguesso, mkutano huo ulihidhuriwa pia na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambae ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Idriss Deby Itno wa Chad pamoja na Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Algeria iliwakilishwa na waziri mkuu wake na Misri na umoja wa mataifa viliwakilishwa pia kwenye mkutano huo wa siku moja uliofanyika kaskazini mwa Congo-Brazzaville.

 Mkutano huo ni wa mara ya pili baada ya mkutano wa kimataifa wa mjini Berlin kuhusu Libya uliofanyika mwezi januari.

Waziri mkuu wa Algeria Abdelaziz Djerad alisema katika mkutano huo, kuwa wakati umewadia  wakuwaweka pamoja Walibya ili wapate ufumbuzi wa mzozo wao. Algeria ndiyo  ilipendekeza kuandaliwa mazungumzo hayo.

 Kwa upande wake rais wa Chad ,Idriss Deby alisema kwamba mzozo wa Libya unaendelea kuzorotesha usalama wa ukanda mzima wa sahel huku ukiingiliwa na wanajeshi kutoka nje.

Naye rais wa Afrika ya Kusini Cyril Ramaphosa ambae pia ni mwenye kiti wa umoja wa afrika, alisema ikiwa mwaka wa kauli mbiu ya ''nyamazisha silaha barani afrika''  nchi za kiafrika zinatakiwa kuwa kwenye mustari wa mbele katika kurejesha amani nchini Libya kwa kuzileta kwenye meza ya mazungumzo pande zote hasimu.

 Kwenye kikao cha kila mwaka mjini Addis-Abeba mwezi uliopita ,viongozi wa Umoja wa Afrika walisisitiza kuwa watachukuwa jukumu muhimu zaidi katika kutanzua migogoro inayoendelea katika bara hilo.