1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arsenal, AC Milan na Marseille zaingia vitani hii leo

23 Novemba 2010

Ligi ya mabingwa barani Ulaya inatimua tena vumbi, huku Arsenal, AC Milan na Olympique Marseille zikiwania tiketi ya duru ijayo ya mtoano.

https://p.dw.com/p/QFr2
Ligi ya mabingwa Barani UlayaPicha: AP/DW

Timu hizo tatu, zinatafuta nafasi hiyo kuungana na Chelsea, Real Madrid pamoja na Bayern Munich ambazo tayari zimekwishafuzu kwa duru hiyo ijayo inayoshirikisha timu 16.

Fußball Champions League - AC Milan - Real Madrid
Mshambuliaji wa AC Milan Mbrazil RonaldinhoPicha: AP

AC Milan ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi lake la G inahitaji kushinda mechi yake hii leo dhidi ya Auxerre, lakini huku ikiomba  vinara Real Madrid iifunge Ajax Amsterdam.

Marseille wao wanahitaji ushindi wa bao zaidi ya moja kwa bila dhidi ya Spartak Moscow ili kujipatia tiketi hiyo.  Arsenala wao ambao ndiyo vinara wa kundi lao H wakitofautiana mabao na Shakhtar Donetsk wanahitaji sare ya aina yoyote ile ili watakapoumana na Spartag Brag,Na Donetsk wataweza pia kufuzu iwapo watapata matokeo mazuri kuliko Brag.

 Nayo AS Roma itaweza kufuzu tu iwapo itaifunga Bayern Munich mjini Roma hii leo, lakini wakati huo huo iombe mungu CFR Cluj and Basel zitoke sare.Bayern yenyewe imekwishafuzu, kwa duru ijayo na pengine inachohitaji ni kushinda ili kukamata uongozi wa kundi hilo.

Mechi za Kundi A,B,C na D zitafanyika kesho Jumatano

Mwandishi:Aboubakary Liongo