1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
WM 2014 Spiel um Platz drei Brasilien Niederlande
Wachezaji wa timu ya taifa ya BrazilPicha: Reuters

Argentina huenda isifike Urusi mwakani

Sekione Kitojo
13 Oktoba 2017

Hatima ya Argentina kuamuliwa kesho Jumanne(10.10.2017)iwapo itaonekana katika fainali za kombe la dunia nchini Urusi. Misri ni timu ya pili kutoka bara la Afrika kujihakikishia nafasi ya kucheza kombe la dunia mwakani.

https://p.dw.com/p/2lWPz

Brazil itafanyia  mabadiliko  kikosi  chake kwa  ajili  ya  michezo  ya kuwania  kukata  tikiti  kwa  kundi  la  mataifa  ya  Amerika ya kusini , ambayo yaelekea  Chile  huenda  ikakaa  nje  ya  fainali  hizo mwaka ujao. Kocha  wa  Brazil Tite alimtumia  mlinda  mlango Ederson  na mlinzi Maeguinhos katika  kikosi  chake  kikuu  wakati  wa  mazowezi mjini  Sao Paulo jana  Jumapili.

Brazil  inayoongoza  michuano  hiyo  ya  America  ya  kusini ilishakata  tikiti  yake  tangu mapema  mwezi  Machi mwaka  huu. Uruguay, Chile, Colombia, Peru, Argentina na  paraguay bado zinategemea  matokeo  ya  kesho  Jumanne  ili  kujihakikishia  uhai ama  kufuzu  katika  fainali  hizo.

Interaktiver WM-Check 2014 Mannschaft Chile
Timu ya taifa ya ChilePicha: picture alliance/AP

Mshambuliaji  wa  Brazil  Gabriel Jesus  amesema  timu  yake haitaionea  huruma  Chile. "Tulicheza  michezo  mitatu  ya  kufuzu tangu  tulipokata  tikiti  yetu kwenda  Urusi  na  tabia  ya  kikosi chetu  imekuwa  ile  ile ,"  amesema  Jesus baada  ya  mazowezi. "tutacheza  ili  kushinda."  ameongeza.

"Iwapo Chile  iko katika  hali  hiyo, sio  kosa  letu, ni  lao," Miranda alisema.

Argentina  nayo  imo  katika  hali  mbaya ,  na  inawezekana mashabiki  wasimuone  Lionel Messi  katika  fainali  hizo. Argentina inakabiliwa  na  kibarua  kigumu  wakati  itakapocheza  na  Ecuador katika  mchezo  mgumu utakaochezwa  katika  mita 2,850 kutoka usawa  wa  bahari  ikiwa  ni  hali  ngumu  kwa  wachezaji  kucheza katika  eneo  ambalo hewa  ni  nyepesi  mno na  kukosa  hewa  ya kutosha.

Fußball WM Qualifikation Argentinien - Uruguay
Lionel Messi huenda hataonekana katika fainali za mwakani 2018Picha: picture-alliance/dpa/N. Aguilera

Syria huenda ikafikia fainali za kombe la dunia

Syria  iko  ukingoni  mwa  kukata  tikiti  yake  katika  fainali  za mwakani  za  kombe  la  dunia  iwapo  itaishinda Australia , baada ya  kutoka  sare  ya bao 1-1 katika  mchezo  wa  kwanza  wa mchujo nchini  Malaysia  wiki  iliyopita. lakini  katika  mchezo huo inabidi kuhimili mashabiki  wa  nyumbani  wa  Australia  ili  kuweza kuendelea  kuwasisimua  mashabiki  wake. Kocha  wa  Australia Ange Postecoglou  hata  hivyo anapanga  mbinu  za  kuwakatisha tamaa  mashabiki  wa  Syria.

"Kile tunachofahamu  ni  kwamba  iwapo  tutashinda  kesho , tutaingia  katika  duru  ijayo na  lengo  letu ni  kucheza  kandanda letu, tunataka  kucheza  kwa  nguvu, tunataka  kushambulia, tunataka kuupeleka  mpira  kwa  maadui zetu na kuwapa changamoto  na hicho  ndio tutakachokifanya."

Australien Ange Postecoglou Trainer
Ange Pestecoglou kocha wa AustraliaPicha: Getty Images/AFP/D. Roland

Katika  bara  la  Afrika  jana  ilikuwa  shangwe  na  vigelegele  kwa mashabiki  wa  Misri baada  ya  kupata  ushindi  wa  mabao  2-1 dhidi  ya  Congo,  ambao  umewapa  tikiti  ya  kucheza  katika  fainali za  kombe  la  dunia nchini  Urusi  kwa  mara  ya  kwanza  tangu miaka  28  iliyopita  nchini  Italia.

Kwa  upande  mwingine katika kundi  hilo  la  E, limeingia  katika  mtafaruku  baada  ya  Ghana iliyotoka  sare  ya  bila  kufungana  na  Uganda  kudai  kwamba  refa wa  mchezo  huo  aliwanyima  bao  pamoja  na  mkwaju  wa  penalti. Ghana  sasa  imeliomba  shirikisho  la  kandanda  duniani  FIFA kufuta  matokeo  hayo  na  kuamuru  mchezo  huo  urudiwe.

Nigeria  yaenda Urusi

Nigeria  imekuwa  nchi  ya  kwanza  ya  Afrika  kukata  tikiti  yake katika  fainali  za  kombe  la  dunia mwakani  baada  ya  kuishinda Zambia  kwa  bao 1-0.

Na  katika mbio  za  marathon  zilizofanyika  jana  Jumapili  mjini Chocago  Galen Rupp  alikuwa  Mmarekani  wa  kwanza  kushinda mbio  hizo  katika  muda  wa  miaka  15  na  Muethiopia Tirunesh Dibaba  akashinda  mbio  hizo  kwa  upande  wa  wanawake. Bingwa wa  medali  ya  shaba  wa Olimpiki  alishinda  mbio  hizo  za  kilometa tano  kwa  muda  bora  wa  masaa  mawili, dakika  tisa na  sekunde 20, akikimbia  marathon  yake  ya  nne.

Olympia London 2012 - Tirunesh Dibaba 10000 m Lauf
Tirunesh Dibaba mkimbiaji kutoka EthiopiaPicha: Reuters

Bingwa  mtetezi  wa  mbio  hizo Abel Kirui  wa  Kenya  alimaliza akiwa  wa  pili kwa  kutumia  masaa  mawili, dakika  9  na  sekunde 48  na  Mkenya  mwingine  Bernard Kipyego  alishika  nafasi  ya tatu.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre / ape / afpe / dpa

Mhariri: Iddi Ssessanga