Ankara. Jeshi laonya kuchukua hatua hatua. | Habari za Ulimwengu | DW | 29.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ankara. Jeshi laonya kuchukua hatua hatua.

Jeshi la Uturuki limesema kuwa liko tayari kuchukua hatua kulinda mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo usioegemea katika dini. Taarifa hiyo imekuja baada ya bunge la Uturuki kufanya uchaguzi wa duru ya kwanza kumchagua rais mpya. Upande wa upinzani umesusia uchaguzi huo ambapo waziri wa mambo ya kigeni Abdullah Gul wa chama cha AK alikuwa mgombea pekee.

Msemaji wa baraza la mawaziri amepuuzia mawazo hayo ya jeshi, kwamba chama cha AK ambacho kina mizizi yake katika Uislamu , kinaweza kutishia katiba ya nchi hiyo ambayo inatenganisha dini na siasa. Ujerumani , ambayo inashikilia urais wa umoja wa Ulaya , imelitaka jeshi la Uturuki kutoingilia katika hatua za kidemokrasia nchini humo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com