1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ahmadinejad azindua ndege iliyotengenezwa Iran

22 Agosti 2010

Rais wa Iran,Mahmoud Ahmadinejad hii leo amezindua ndege ya masafa marefu inayoweza kupachikwa mabomu.

https://p.dw.com/p/OtcQ
This photo released by the Iranian Defense Ministry, shows Iranian President Mahmoud Ahmadinejad, as he speeches during a ceremony of inauguration of the Karrar, or striker in Farsi, which the Iran claims is the first domestically-built, long-range, unmanned bomber aircraft, at the Malek-e Ashtar University on Sunday, Aug. 22, 2010. Iranian President Mahmoud Ahmadinejad Sunday inaugurated the country's first domestically-built, long-range, unmanned bomber aircraft, calling it an "ambassador of death" to Iran's enemies. (AP Photo/Iranian Defense Ministry,Vahid Reza Alaei, HO) ** EDS NOTE: THE ASSOCIATED PRESS HAS NO WAY OF INDEPENDENTLY VERIFYING THE CONTENT, LOCATION OR DATE OF THIS IMAGE. **
Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad akitoa hotuba wakati wa sherehe za kuizindua ndege ya kubeba mabomu iliyotengenezwa Iran.Picha: AP

Ndege hiyo yenye urefu wa mita nne imeonyeshwa hadharani siku moja baada ya kufunguliwa kituo cha nyuklia cha Bushehr kusini mwa nchi.

Kwa mujibu wa ripoti za televisheni ndege hiyo inayoruka bila ya rubani inaweza kubeba mabomu ya aina mbali mbali na kwenda masafa marefu na kwa kasi kubwa.

Ndege hiyo ni sehemu ya mipango ya Iran kutengeneza silaha zake zenyewe badala ya kutegemea nchi za nje. Israel na nchi za magharibi zinatuhumu kuwa Iran ina mpango wa siri kutengeneza silaha za nyuklia, lakini Iran inakanusha tuhuma hizo.

Mwandishi: P.Martin/ZPR

Mhariri: M.Dahman