Vikosi vinavyomtii kiongozi anayeng'ang'ania madaraka nchini Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo vimeyashambulia makao makuu ya mpinzani wake kwa makombora.
Viongozi kutoka nchi za Kiarabu na Ulaya watakutana siku ya Jumapili nchini Saudi Arabia katika mkutano wa kilele wa kiuchumi pamoja na mazungumzo ya Jumatatu yatakayojadili vita vya Gaza.
Ligi Kuu ya Kandanda hapa Ujerumani - Bundesliga inaelekea ukingoni. Baada ya bingwa kujulikana sasa macho yote yamegeuka katika nafasi za kucheza kandanda la Ulaya. Kwa mengi zaidi kuhusu mechi za wikiendi hii Suleman Mwiru amezungumza na Bruce Amani kuhusu michezo ya wikiendi hii na ambao utatangazwa mubashara kupitia ukurasa wa Facebook wa DW Kiswahili na kupitia redio mbalimbali washirika.
Rais wa China Xi Jinping amemuambia Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Antony Blinken, kwamba pande hizo mbili zinapaswa kuwa washirika kwenye masuala mbalimbali ya kikanda na kilimwengu na sio kuwa washindani.