Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Deo Kaji Makomba amepata nafas ya kuzungumza na vijana waliothirika wa madawa ya kulevya walioko katika kituo cha kuwabadilisha Tabia cha Tasol mjini Dodoma, Tanzania. Je imekuaje wakaingia katika janga hili na wamefanikiwa vipi kujiokoa katika tatizo hili? Vijana Tugutuke inajibu masuali yote haya. Nenda kwenye sauti
Katika kipindi hiki cha vijana mchaka mchaka Sylvia mwehozi anaangalia ajira tofauti kwa vijana zinazotokana na katika shughuli za harusi barani Afrika. Ni kwa kiasi gani kazi hizo zimeleta tofauti katika maisha ya vijana? Sylvia Mwehozi anakueleza zaidi. Nenda kwenye sauti
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ndiye mwenyekiti mpya wa EAC/ Hali ya COVID 19 ikoje mpakani mwa Burundi na Tanzania?/ Human Rights Watch yataka Sudan ikomeshe kamatakamata/ Suu Kyi afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka mapya/ Trump afikiria kuwania tena Urais 2024 Nenda kwenye sauti
Mashirika katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma huko Turkana, Kenya yanavyofanya kazi ya ziada kuboresha mazingira ya kambi hiyo. Mashirika hayo yanakusanya taka za plastiki ambazo baadaye zinatumika kutengeza bidhaa mbalimbali. Fuatana naye Michael Kwena katika video hii kufahamu zaidi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ndiye mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, akichukua mikoba hiyo kutoka kwa rais wa Rwanda Paul Kagame. Lakini changamoto katika jumuiya hiyo ni tele ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa asasi zake, migawanyiko na hata kuhoji umuhimu wake. Zaidi John Juma amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Dar es Salaam Abdulkadir Atiki.
Watu 18 wauawa katika maandamamo Myanmar Trump: Huenda nikawania tena Urais 2024 Rais wa zamani wa Ufaransa kujua hatma yake juu ya kesi ya ufisadi inayomkabili
Watu 18 wauawa katika maandamamo Myanmar//Trump: Huenda nikawania tena Urais 2024//Rais wa zamani wa Ufaransa kujua hatma yake juu ya kesi ya ufisadi inayomkabili
Watu 18 wauawa katika siku mbaya ya umwagaji damu Myanmar, Navalny kuanza kutumikia kifungo chake katika jimbo la Vladimir na Ufaransa yazungumza na Ujerumani kuhusu vizuizi vya usafiri vilivyotangazwa na Ujerumani baada ya wasiwasi wa kusambaa kwa ugonjwa wa COVID 19 katika eneo la ufaransa la Moselle.
Watu watano wameuwawa katika makabiliano ya polisi Myanmar, Wanaharakati 47 wakamatwa kwa makosa ya kufanya uasi Hong Kong na Rais wa Marekani Joe Biden kutoa tamko kuhusu Saudi Arabia siku ya Jumatatu
Karibu katika matangazo ya asubuhi ikiwa ni tarehe ya mwisho ya Mwezi Februari. Tumekuandalia makala za Mtu na mazingira, utamaduni na sanaa na nyinginezo
Marekani yaidhinisha chanjo ya tatu kwa matumizi ya dharura. Myanmar yamfuta kazi balozi wake wa Umoja wa Mataifa. Wanafunzi na walimu waliotekwa nyara kaskazini mwa Nigeria waachiwa huru.
Uamuzi wa rais Joe Biden wa kutomwadhibu mrithi wa mfalme wa Saudi Arabia kwa mauaji ya mwandishi habari Jamal Khashoggi wawavunja moyo wanaharakati, Iran yasema mashambulizi ya angani yaliofanywa Ijumaa na Marekani Mashariki mwa Syria yanachochea ugaidi na Spika wa bunge nchini Libya Aguila Saleh asema bunge kuzungumzia kura ya kutokuwa na imani na serikali mpya ya umoja wa taifa Machi 8
Israeli yatakiwa kusimamisha ubomoaji wa makazi ya Wabedouin katika Bonde la Jordan, waziri wa mambo ya nje wa Bangladesh A.K. Abdul Momen asema nchi yake haina wajibu wa kutoa hifadhi kwa wakimbizi 81 wa jamii ya waislamu ya Rohingya na Saudi Arabia yakanusha ripoti ya Marekani kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo Mohammed bin Salman aliidhinisha mauaji ya Jamal Khassogi
Serikali ya Saudi Arabia yakanusha mwanamfalme Mohammed Bin Salmin kuagiza kuuliwa kwa Jamal Khashoggi. Syria na Iran zimelaani shambulizi lililofanywa na Marekani jana dhidi ya wapiganaji wenye silaha. Zaidi ya wafungwa 400 wametoroka jela nchini Haiti.
Wanaharakati washutumu jeshi la Uganda kwa ukiukaji wa haki// Makundi ya vijana yaungana Kenya dhidi ya uhalifu// Ripoti inatarajiwa kuchapishwa na shirika la kijasusi la Marekani kuhusiana na kuhusiana na ushiriki wa mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman katika mauaji ya kikatili ya mwandishi habari Jamal Khashoggi.
Sakata la janga la corona nchini Tanzania, kuuwawa kwa balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mjini Goma, kizungumkuti cha tarehe ya uchaguzi nchini Somalia na hali huko Cameroon ni miongoni mwa yaliyotawala Afrika Wiki Hii na msimulizi ni Sylvia Mwehozi.