Kansela Angela Merkel amesema atagombea muhula wa nne katika uchaguzi mkuu wa mwakani. Bi Merkel ametoa tangazo hilo mjini Berlin akisimama mbele ya bango la Chama chake cha Kihafidhina, Christian Democratic Union, CDU. Nenda kwenye makala
Bonyeza hapa kusoma Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW
Rais wa Marekani Barack Obama ametetea ushirikiano wa biashara huria wa kiuchumi wa mataifa ya Asia na Pacific APEC
Shirika la kimataifa la haki za binadamu, la Human Rights Watch, limetoa picha za satelaiti Jumatatu (21.11.2016) zinazoonyesha uharibifu mkubwa kwenye jimbo la Rakhine lililopo nchini Myanmar.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani Jumapili (21.11.2016) amethibitisha kwamba atagombania tena ukansela katika uchaguzi wa mwaka 2017.
Watu zaidi ya 100 wameuwawa na wengine zaidi 150 wamejeruhiwa wakati treni ilipoacha reli katika jimbo la Uttar Pradesh kaskazinii India Jumapili (20.11.2016) wakati juhudi za kutafuta manusura zikiendelea
Waendesha mashitaka nchini Korea Kusini wanasema wanaamini Rais Park Guen-hye alikula njama na mshirika wake mkubwa, ambaye alitumia mafungamano yake na rais huyo kujipatia utajiri mkubwa usiokuwa na maelezo.
Marekani imewasilisha pendekezo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuiwekea Sudani Kusini vikwazo vya biashara ya silaha kufuatia onyo kuwa nchi hiyo iko katika hatari ya kuingia kwenye mauaji makubwa.
Waandamanaji wamekusanyika nje ya mahakama nchini Afrika Kusini kupinga ubaguzi, ambapo raia wawili weupe wanakabiliwa na mashitaka ya kumshindilia kwa nguvu raia mweusi katika jeneza na kumtishia kumchoma.
Morocco ndiye mwenyejii wa mkutano wa kilele wa viongozi wa Afrika katika wakati ambapo taifa hilo likijaribu kurejea kuwa mwanachama wa Umoja wa Afrika baada ya kujiondoa miaka 32 iliyopita.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, anasema zaidi ya bunduki 5,200 zimeteketezwa kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki katika jitihada za kuzuia mzunguko wa silaha kuyafikia makundi ya kihalifu.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, amesema hana mpango wa kung'ang'ania madaraka. Ameahidi kuwa uchaguzi mkuu utafanyika ndani ya miezi michache badala ya mwishoni mwa mwaka 2016.
Umoja wa Mataifa una wasiwasi juu ya sheria mpya kuhusu vyombo vya habari vya kigeni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo vimetakiwa kurusha matangazo yao chini ya vituo vya ndani vinavyokubalika
Karibu mataifa 200 yamekubaliana kutengeneza ndani ya kipindi cha miaka miwili sheria za kuutekeleza mkataba wa kihistoria wa kimataifa uliotiwa saini mwaka wa 2015 ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Mkutano wa UN huko Marrakesh, Morocco unafikia kikomo hii leo huku kukiwa na hofu kuwa lengo la kuzuia mabadiliko ya tabia nchi huenda lisiafikiwe iwapo hakutakuwa na uungwaji mkono kutoka Marekani.
Viongozi wa nchi, biashara na wanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani wamemtaka Rais mteule wa Marekani Donald Trump kutoindoa nchi hiyo katika mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa uliofikiwa Paris.
Serikali ya Kenya imesema kwamba imeamua kuchelewesha kufungwa kwa kambi ya wakimbizi ya Dadaab ambayo inaichukulia kuwa tishio la usalama, baada ya shinikizo la kimataifa la kutaka kuwapa wakimbizi hao muda zaidi
Kiasi ya watu 600,000 wanakabiliwa na uhaba wa chakula nchini Burundi kutokana na ukame na mafuriko katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na idadi hiyo inaweza kuongezeka hadi kufikia 700,000 kwa mwaka ujao.
Andy Murray amemwonya Novak Djokovic kuwa yuko tayari kuendeleza udhibiti wake kileleni mwa mchezo wa tennis baada ya Mscotland huyo alikamilisha msimu wake katika nafasi ya kwanza ulimwenguni
Mabingwa watetezi Real Madrid, Barcelona, Manchester City na Juventus ni miongoni mwa timu zinazoweza kujikatia tikiti ya hatua ya 16 za mwisho katika michuano ya wiki hii ya makundi katika Champions League
Tuma Facebook Twitter google+ Whatsapp Tumblr Digg Newsvine
Kiungo http://dw.com/p/2T1Mo
Kansela Angela Merkel atangaza atawania muhula wa 4. Watu 142 wafariki kwenye ajali ya treni India. Nicolas Sarkozi ashindwa katika mchujo wa urais na Haiti yapiga kura kuchagua rais. Papo kwa Papo 21.11.2016
Kiungo http://dw.com/p/2Su9E
Obama akutana na viongozi wa EU, Marekani yataka Sudan Kusini kuwekewa vikwazo vya silaha lakini Urusi na China zapinga, wahamiaji haramu 200 kutoka Burundi wakamatwa Tanzania wakifanya kazi kinyume cha sheria. Papo kwa Papo 18.11.2016
Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com
Kiungo http://dw.com/p/2SSau
Dar es Salaam, jiji kuu la kiuchumi na kibiashara nchini Tanzania, Mohammed Khelef alikutana na vijana wanaoshajiisha na kujihusisha na ujasiriamali jamii kupitia mitandao ya kijamii inayowakutanisha na mamilioni ya wenzao kote duniani
Kiungo http://dw.com/p/2SSbU
Nini nafasi ya mitandao hii kwenye kubadili maisha ya vijana wa Kiafrika na kuwafanya kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha yao? Mjini Nairobi, Mohammed Khelef alikutana na mwanablogu maarufu Robert Alai, na hapa anazungumzia kile ambacho mitandao ya kijamii inamaanisha kwake na kwa jamii ya vijana wa Kenya
Kiungo http://dw.com/p/2SSbX
Mohammed Khelef akutana na vijana wa jijini Nairobi wanaotumia mitandao ya kijamii kuhamasishana katika kilimo salama kwenye maeneo ya mijini kupitia kampeni wanayoiita “Adilisha“
Kiungo http://dw.com/p/2SSbZ
Shirika la Jamii Media ambalo linaendesha mtandao wa kijamii wa Jamii Forum linasimamia hivi sasa mradi wa kufuatilia utekelezaji ahadi za wanasiasa waliochaguliwa kwa kura majimboni kwa kutumia mitandao ya kijamii unaoitwa Tushirikishane
Kiungo http://dw.com/p/2SSbV
Katika mji wa kitalii wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania, vijana wanaotokea asasi za kijamii na za kibiashara zinazoyalenga makundi maalum ya kijamii, mitandao ya kijamii imekuwa kila kitu kuhusu maisha yao
Kiungo http://dw.com/p/2Sicr
Mitandao ya kijamii inajenga mtandao baina ya watu na inawaleta karibu zaidi hata wale walio mbali.
Kiungo http://dw.com/p/2SSbW
Mwenzangu Mohammed Khelef amezungumza na George Akilimali, mwanzilishi wa Kampuni ya SmartCore Social Enterprise, inayojihusisha na uwezeshaji wa vijana katika kuifikia teknolojia, jijini Arusha, kaskazini mwa Tanzania, juu ya dhana ya "uchumi wa mitandao ya kijamii".
Kiungo http://dw.com/p/2Sp03
Alama unazowacha mtandaoni ni tafsiri inayoelezea wewe ni nani na watu huenda wakakutafsiri kwa alama hizo.
Bonyeza hapa kupata mukhtasari wa habari muhimu duniani katika video fupi za 'Papo Kwa Papo'