DW: Katika Premier League leo, Liverpool itavaana na Tottenham Hotspur, ambapo Tottenham inatafuta nafasi ya kubakia nyuma ya Manchester City na Manchester United.
Kocha wa Manchester United Erik ten Hag amesema kwamba mchezaji Jadon Sancho "anajua anachopaswa kufanya" ikiwa anataka kuokoa kibarua chake ndani ya Old Trafford.
Baada ya mashtaka ya kujaribu kubaka kutupiliwa mbali, Manchester United imekuwa ikifanya uchunguzi wao wenyewe kuhusu Mason Greenwood. Kabla ya msimu mpya, mashabiki wa United waliandamana kupinga kurejea kwa Greenwood.
Jitihada za muda mrefu za kocha Pep Guardiola kushinda tena Ligi ya Mabingwa Ulaya zilifikia mwisho jana jusiku wakati Manchester City hatimaye walitwaa ubingwa wa Ulaya.