1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Ten Hag asema mlango bado uko wazi kwa Sancho United

9 Desemba 2023

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag amesema kwamba mchezaji Jadon Sancho "anajua anachopaswa kufanya" ikiwa anataka kuokoa kibarua chake ndani ya Old Trafford.

https://p.dw.com/p/4ZyGm
Winga wa Manchester United Jadon Sancho
Winga wa Manchester United Jadon SanchoPicha: Jon Super/AP Photo/picture alliance

Sancho, ambaye aliigharimu United pauni milioni 73 alipohama kutoka Borussia Dortmund mwaka 2021, amekuwa nje ya kikosi cha kocha Ten Hag tangu mwezi Septemba na kuambiwa afanye mazoezi peke yake baada ya kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefanywa kile alichokitaja kama kisingizio na meneja wake.

Ten Hag amesema ni utamaduni na kila mchezaji lazima alingane na viwango. Sancho amefunga mabao 12 katika mechi 82 alizoichezea United lakini kukosekana kwake kumefungua milango kwa Alejandro Garnacho kushiriki mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni.