1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika waendelea kusaka suluhu Burundi

Mohamed Abdul-Rahman26 Februari 2016

Ujumbe wa Umoja wa Afrika unaowajumuisha marais watano uko mjini Bujumbura kwenye ziara ya siku mbili inayolenga kuumaliza mgogoro mkubwa wa kisiasa unaoikumba Burundi.

https://p.dw.com/p/1I2ke
Ujumbe wa Rais Jacob Zuma ukiwasili mjini Bujumbura.
Ujumbe wa Rais Jacob Zuma ukiwasili mjini Bujumbura.Picha: Reuters/E. Ngendakumana

Ujumbe huo unaongozwa na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akiandamana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Haile Mariam Deseleyn, na marais wa Alli Bongo Ondimba wa Gabon, Mohamed Ould Abdelaziz wa Mauritania na Macky Sall wa Senegal.

Kilichowashangaza wengi mjini Bujumbura ni hatua ya Zuma kuwasili akilindwa na walinzi wake wapatao 50 kutoka nchini mwake wakiwa kwenye magari sita ya kijeshi.

Wakati huo huo, wapinzani waishio uhamishoni wameeleza kukasirishwa kwao na kauli ya Rais Pierre Nkurunziza kuwa hatazungumza na wale aliowaita "magaidi" anaowatuhumu kushiriki katika vitendo vya kuvuruga usalama.

Mazungumzo ya awali yalikwama baada ya serikali ya Burundi kukataa kukaa meza moja na wapinzani inaowahusisha na jaribio la kijeshi lililoshindwa mwezi Mei mwaka jana.