1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Zelensky amfuta kazi mlinzi baada ya jaribio la kumuuwa

10 Mei 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemfuta kazi mkuu wa idara inayohusika na ulinzi wake, baada ya maafisa wawili katika idara hiyo kukamatwa wiki hii kuhusiana na madai ya jaribio la kutaka kumuua rais huyo

https://p.dw.com/p/4fhKa
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais Zelensky alimfuta kazi mkuu wa idara ya ulinzi wake, baada ya kukamatwa maafisa wawili kwa njama ya kumuuwaPicha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance

Amri ya Zelenskiy ya kumwachisha kazi Sergiy Leonidovich Rud haikutaja sababu ya hatua hiyo wala mtu atakayeichukua nafasi yake katika wadhfa huo wenye umuhimu mkubwa.

Soma pia: Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana

Tangazo hilo limetolewa ikiwa ni siku chache baada ya idara ya usalama ya Ukraine SBU kutangaza kwamba, imezima jaribio la Urusi la kumuua Zelenskiy na maafisa wengine waandamizi serikalini. SBU iliongeza kuwa inawashikilia makanali wawili inaowashuku walivujisha taarifa kwa shirika la usalama la Urusi FSB.

Katika hatua nyingine Ukraine na Urusi zimeendelea kushambuliana kwa kutumia ndege za Droni katika mashambulizi ya usiku kucha.