1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky ahudhuria mkutano Berlin

11 Juni 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky yupo mjini Berlin kuhudhuria mkutano juu ya kuimarisha misaada ya kuichumi kwa ajili ya kuijenga upya nchi yake.

https://p.dw.com/p/4gthG
Volodymyr Zelensky mjini Berlin Ujerumani
Volodymyr Zelensky mjini Berlin UjerumaniPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Wajumbe zaidi ya 2000 kutoka nchi 60 wapo mjini Berlin kwa ajili ya mkutano huo.Wajumbe hao watajadili njia za kuwezesha juhudi za kimataifa katika kuiunga mkono Ukraine kwa kuitekeleza mipango ya muda mrefu. 

Akiufungua mkutano huo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema nchi yake itashirikiana na washirika wake katika utoaji sawa wa mitaji kwa kampuni za Ukraine.

Scholz amezihimiza kampuni binafsi kuwekeza fedha katika kuijenga upya Ukraine, na amehamasisha misaada zaidi kutoka kwa jamii ya kimataifa kwa ajili ya ujenzi mpya wa Ukraine baada ya vita.

Huo ni mkutano wa tatu tangu kuzinduliwa mnamo mwaka 2022 baada ya Urusi kuivamia Ukraine.