1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zawadi ya Putin kwa Kim Jong Un yakosolewa na wanaharakat

20 Februari 2024

Waangalizi wanasema kitendo cha rais wa Urusi Vladimir Putin kumzawadia gari ya kifahari kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kunakiuka azimio la Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4cdDc
Kim na Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: Vladimir Smirnov/AFP

Azimio hilo la Umoja wa Mataifa linapiga marufuku kusafirisha bidhaa za thamani nchini humo.

Vikwazo hivyo dhidi ya Pyongyang vilichukuliwa katika jaribio la kuishinikiza nchi hiyo kuachana na mpango wake wa silaha za nyuklia. 

Zawadi hii ya Putin inadhihirisha kwa mara nyingine kukua kwa ushirikiano kati ya Urusi na Korea Kaskazini katika dhamira ya kupambana na adui wao mmoja ambaye ni Marekani na washirika wake.