1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar kutumia ndege zisizo na rubani kupambana na Malaria

Bruce Amani
5 Novemba 2019

Kwa mara ya kwanza ndege zisizoruka na rubani zinafanyiwa majaribio ya kusaidia kupambana na malaria visiwani Zanzibar. Ndege hizo zitanyunyiza kemikali aina ya Aquatain kwenye mashamba ya mpunga.

https://p.dw.com/p/3SUC9
Drohne über einen Feld
Picha: picture-alliance/Photoshot/Z. Xudong

Kwa mara ya kwanza ndege zisizoruka na rubani zinafanyiwa majaribio ya kusaidia kupambana na malaria visiwani Zanzibar. Ndege hizo zitanyunyiza kemikali aina ya Aquatain kwenye mashamba ya mpunga ambayo yana maji mengi yanayowapa mazingira mazuri ya kutaga mayai mbu wanaosababisha malaria. Inatarajiwa kuwa mbinu hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya mbu wanaosambaza ugonjwa wa Malaria katika eneo hilo. Unyunyiziaji huo wa ndege zisizo na rubani ni jaribio la kuona kama itaisaidia serikali ya Zanzibar kufikia lengo lake la kuangamiza malaria visiwani humo ifikapo 2023, kwa mujibu wa mpango wa kimkakati ulioidhinishwa na Programu ya Kuangamiza Malaria Zanzibar.