1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Zaidi ya watu 50,000 wakimbia mji mkuu wa Haiti

Tatu Karema
3 Aprili 2024

Zaidi ya watu 53,000 wamekimbia mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika wiki tatu za mwezi Machi wakati vurugu za magenge yenye silaha ziliposababisha uharibifu mkubwa kwa raia

https://p.dw.com/p/4eMrc
Polisi washika doria mjini  Port-au-Prince nchini Haiti kutokana na ghasia za magenge ya uhalifu
Polisi washika doria mjini Port-au-Prince nchini HaitiPicha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Makadirio ya Umoja wa Mataifa yaliotolewa siku ya Jumanne, yanaonesha kuwa maelfu ya watu waliondoka mjini Port-au-Prince kati ya Machi 8 na 27 huku ghasia zikizuka tena wikendi ya Pasaka na mwanzoni mwa mwezi Aprili.

Unyanyasaji wa haki za binadamu Haiti wafikia viwango vya kutisha

Mkuu wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Volker Turk, amesema kuwa unyanyasaji wa haki za binadamu ulikuwa unafanyika katika kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na uhalifu wa kingono.

Soma pia:Mexico yawahamisha raia wake 34 kutoka Haiti

Mzozo huo pia umezuia kusafirishwa kwa bidhaa muhimu na misaada ya kibinadamu katika mji huo mkuu.

Watu wengi wanahamia upande wa Kusini wa Haiti

Kulingana na Umoja wa Mataifa, watu wengi waliopoteza makazi wanasafiri kuelekea rasi ya Kusini ya nchihiyo ambayo bado inajikwamua kutokana na tetemeko kubwa la ardhi la mwaka 2021.