1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMexico

Mexico yawahamisha raia wake 34 kutoka Haiti

Tatu Karema
2 Aprili 2024

Mexico imewahamisha raia wake 34 kutoka Haiti kwa kutumia meli ya kijeshi kutokana na hali mbaya ya usalama inayozidi kukithiri nchini humo. Haya yametangazwa Jumatatu na serikali ya nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4eK4h
Wanajeshi washika doria mjini Port -au-Prince mnamo 13.03.2024, baada ya kuzuka kwa ghasia za magenge nchini Haiti
Wanajeshi washika doria mjini Port -au-PrincePicha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Katika mkutano na wanahabari, waziri wa mambo ya nje wa Mexico Alicia Barcena, amesema kuwa watoto saba na maafisa wanne wa kidiplomasia waliokuwa wakazi wa Haiti ni miongoni mwa waliohamishwa.

Soma pia:Mtaalam wa UN: Haiti inahitaji walinda amani 5,000 kukabiliana na magenge ya wahalifu

Serikali ilionyesha picha za raia wa Mexico wakipanda helikopta ili kupelekwa kwenye meli hiyo, kutokana na kufungwa kwa uwanja wa ndege waPort-au-Prince.

Barcena ameongeza kuwa operesheni maalumu ilihitajika kuwaokoa watu hao ambao tayari wako safarini kuelekea Mexico.

Haiti imekumbwa na machafuko tangu mwezi Februari

Haiti imekumbwa na mapigano yanayozidi kuongezeka tangu mwishoni mwa mwezi Februari, wakati magenge yenye silaha yalipoanzisha mashambulizi yaliyoratibiwa na kumtaka waziri mkuu Ariel Henry kujiuzulu.