1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Zaidi ya watu 30 wauawa Somaliland

6 Februari 2023

Watu 34 wameuawa katika mapigano yaliyozuka kwenye mkoa wa Somalia uliojitenga wa Somaliland.

https://p.dw.com/p/4N9WF
Markt in Somalia
Picha: picture alliance/Africa 24 Media/Tim Freccia

Mapigano yalizuka mashariki mwa Somaliland asubuhi ya leo kati ya vikosi vya mkoa na wapiganaji wanaoipinga serikali, mwezi mmoja baada ya watu wapatao 20 kuuawa katika maandamano kuhusu udhibiti wa maeneo yanayozozaniwa.

Mohamed Farah, daktari katika hospitali ya Laascaanood, katika mkoa wa Sool, amesema watu wasiopungua 34 wameuawa na wengine 40 wamejeruhiwa katika mapigano ya leo. Farah amesema aliona miili ikiletwa hospitalini.

Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991, lakini uhuru wake haujatambuliwa kimataifa, na imeshuhudia upinzani mkubwa dhidi ya madai yake juu ya ardhi kwenye mpaka wa mashariki na Puntland, ambao ni mmoja ya mikoa ya Somalia yenye utawala wake wa ndani.