1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF: Mtoto 1 kati ya 4 anakabiliwa na ukosefu wa chakula

6 Juni 2024

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limesema leo kwamba zaidi ya mtoto mmoja kati ya wanne wa chini ya miaka mitano kote ulimwenguni anakabiliwa na umasikini wa hali ya juu wa chakula.

https://p.dw.com/p/4ghva
Mama akimnyonyesha mtoto wake
Mtoto akinyonya maziwa. Watoto wengi hivi sasa wanakabiliwa na kitisho cha ukosefu wa chakula cha kutosha dunianiPicha: picture alliance/BSIP

Kulingana na UNICEF, idadi hiyo inamaanisha kwamba zaidi ya watoto milioni 180 wanakabiliwa na kitisho cha kuathirika katika ukuaji.

Mkuu wa UNICEF Catherine Russell amesema watoto wanaokula makundi mawili tu ya chakula kwa siku kama wali na maziwa wana uwezekano wa zaidi ya asilimia 50 wa kupata aina mojawapo ya utapiamlo mkali.

Umaskini mkubwa wa chakula kwa watoto umekithiri katika nchi kama 20, na hasa Somalia, ambapo asilimia 63 ya watoto wadogo wameathirika; Guinea, Guinea-Bissau na Afghanistan.