Westerwelle ziarani India | Matukio ya Kisiasa | DW | 19.10.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Westerwelle ziarani India

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle yuko India katika ziara yake ya kwanza nchini humo tangu kuchukua wadhifa huo mwaka mmoja uliopita.

Waziri wa Nje wa India S.M. Krishna, kushoto, na mgeni wake Guido Westerwelle wa Ujerumani

Waziri wa Nje wa India S.M. Krishna, kushoto, na mgeni wake Guido Westerwelle wa Ujerumani

Ziara ya Westerwelle katika nchi hii yenye demokrasia kongwe kabisa duniani, pamoja na idadi kubwa ya wakaazi ni mambo yanayomvutia sana.

Waziri anatambua hamasa walioyonayo raia wa nchi hii katika kujishughulisha, pamoja na ukuaji wa uchumi, na pia katika hali mnyumbuliko ya nchi hiyo. Hayo yote anayatambua.

Ni lazima mtu , anapoangalia dunia , kutambua , ni kiasi gani nchi zinavyojaribu kujitokeza kwa kasi na zinavyotaka kupanda juu, hili linapaswa kutambuliwa.

Westerwelle hana maneno zaidi ya kuisifu India na juhudi zake za kujiimarisha duniani.

Baada ya mazungumzo na waziri mwenzake pamoja na waziri mkuu, ameitaka India kuchukua jukumu la mbele katika ulinzi wa mazingira pamoja na kushughulikia mizozo ya kimkoa, akitambua wazi kuwa , kutokana na maslahi yake ya kiuchumi ulinzi wa mazingira kwa India ni suala gumu.

India ni sehemu muhimu ya nguvu za demokrasia inayoleta uthabiti katika eneo la Asia, na ndio sababu tunahitaji kuimarisha ushirika na India.

Maadili haya ya pamoja ndio msingi wa hatua za kufanyakazi kwa pamoja kati ya India na Ujerumani, pamoja na mkakati wa ushirika wetu.

Mkakati wa ushirika na India unaweza kujaribiwa katika baraza la usalama la umoja wa mataifa, kwa kuwa nchi zote mbili ni wanachama ambao si wa kudumu wa baraza la usalama la umoja huo, na nchi zote zinataka mageuzi katika umoja wa mataifa.

Kwa hilo hata hivyo waziri Westerwelle anachukua tahadhari sana. Amesema kuwa suala la mageuzi katika umoja wa mataifa si suala la nchi gani ina nguvu sana katika baraza la usalama ama ipi ni dhaifu, suala ni ulazima wa kuufanyia mageuzi umoja wa mataifa ili kuufanya kuwa na nguvu zaidi.

Pia waziri Westerwelle amesema baada ya mazungumzo na waziri mkuu Manmohan Singh na waziri wa mambo ya kigeni SM Krishna mjini New Delhi kuwa itakuwa ni hatua kubwa mbele iwapo India itatia saini mkataba unaopiga marufuku majaribio ya silaha za kinuklia.

India inapinga hatua kama hiyo, ikisema kuwa makubaliano kama hayo yanaugawa ulimwengu baina ya mataifa yenye silaha za kinuklia na yale ambayo hayana.

Kuhusu suala la Iran waziri Guido amesema kuwa kuna hali ya kukubaliana, kwamba hakuna mtu katika jamii ya kimataifa ambaye anaona kuna maslahi kwa Iran kutumia tekolojia ya kinuklia iliyonayo kwa njia mbadala ya kuunda silaha , mtazamo huu upo kwa serikali zetu zote mbili.

Ziara ya waziri Westerwelle inamalizika leo Jumanne.

Mwandishi : Kostolnik , Barbara / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Aboubakary Liongo.

 • Tarehe 19.10.2010
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PhuY
 • Tarehe 19.10.2010
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PhuY
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com