Wengine wafa katika machafuko mengine Kenya | Habari za Ulimwengu | DW | 29.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wengine wafa katika machafuko mengine Kenya

Takriban watu wengine 15 wameuawa katika ghasia za kikabila magharibi mwa Kenya.Hii inajumulisha vifo vya watu 49 katika kipindi cha saa 24 zilizopita.Polisi inasema vifo vya hivi sasa vimetokea pale nyumba kadhaa zilipochomwa moto na magenge ya watu.Na kwa mda huohuo mwanasiasa wa upande wa upinzani kutoka chama cha Orange Democratic Movement –ODM amepigwa risasi na kuuawa nyumbani kwake na watu wasiojulikana. Haijatambulika baado sababu ya mauaji ya mbunge huyo Mugabe Were,yaliyotokea usiku wa kuamkia leo mjini Nairobi.Mmoja wa viongozi wa ODM Anyang Nyong amesema kuwa kifo cha mbunge huyo ni cha kusikitisha.

Mauaji ya mbunge huyo yamezusha ghasia zingine katika mtaa wa mabanda wa Kibera pamoja na sehemu zingine nchini Kenya.Taarifa zinasema kuwa nyumba kadhaa zimechomwa moto katika mtaa huo wa Kibera karibu na reli inayogawanya jamii za wakikuyu na wa jaLuo.Na mjini Kisumu polisi ilipata maiti moja ambayo imeungua vibaya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com