1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa ulinzi wa Liberia ajiuzulu baada ya siku chache

Sudi Mnette
13 Februari 2024

Waziri mpya wa ulinzi wa Liberia, Prince .C. Johnson amejiuzulu wadhifa wake ikiwa ni siku 10 tu baada ya kuteuliwa, kufuatia maandamano yaliyofanywa na wake wa wanajeshi wa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4cKmB
Rais wa Liberia Joseph Boakai
Rais wa Liberia Joseph Boakai akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters nyumbani kwake Monrovia, Novemba 19, 2023.Picha: Carielle Doe/REUTERS

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais, imesema rais Joseph Boakai, amepokea na kukubali barua ya kujiuzulu waziri huyo. Katika barua yake, Johnson ametaja machafuko ya sasa ya kisiasa na ya kiraia yaliyopelekea maandamano kuwa ni sababu ya kujiuzulu kwake, ambapo ameeleza kuwa amefanya hivyo ili "kulinda amani na usalama wa nchi". Wanawake hao walioandamana waliweka vizuizi barabarani ikiwemo karibu na mji mkuu Monrovia, huku wakimtaka rais Boakai kuboresha masuala kadhaa ikiwemo mishahara ya wanajeshi, na huduma za kijamii. Rais Boakai ambae kwa maandamano haya kuwa ni changamoto ya kwanza tangu aingie madarakani,amewataka watu kuwa watulivu huku akiahidi kuwa serikali yake itashughulikia matatizo yao.