SiasaAsia
Waziri mkuu wa Uhispania afanya ziara nchini China
13 Aprili 2026
Matangazo
Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Tsinghua mjini Beijing leo, Sánchez aliitaka China kutekeleza jukumu kubwa kimataifa, siku moja kabla ya kukutana na rais wa nchini hiyo Xi Jinping.
Sanchez ameongeza kusema China inaweza kufanya mengi kwa mfano kutaka sheria ya kimataifa iheshimiwe pamoja na kusitisha vita nchini Lebanon, Iran, Gaza, Ukingo wa Magharibi na Ukraine.
Ziara yake inakuja katika wakati mgumu wa kisiasa na kijiografia ambapo viongozi wa Ulaya wanajaribu kushawishi kusitishwa kwa vita vya Marekani na Israel nchini Iran, huku mahusiano ya Uhispania na Marekani yakiwa yamedhoofishwa na kauli za Sánchez za kukosoa vita hivyo.