1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Tabia NchiUgiriki

Waziri mkuu wa Ugiriki aunda kikosi maalum kukabili moto

25 Julai 2023

Waziri Mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis, ametetea hatua za kikosi cha kukabili moto wa nyika ambao umeikumba nchi hiyo kwa zaidi ya wiki moja.

https://p.dw.com/p/4UNLy
Griechenland | Neuer Außenminister | Giorgos Gerapetritis
Picha: Giorgos Kontarinis/Imago Images

Katika taarifa yake kupitia televisheni ya taifa, Mitsotakis amesema hakuna suluhu ya miujiza katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kwamba kama kungelikuwa na suluhisho kama hilo wangelitumia. 

Mitsotakis ameendelea kutetea kuhamishwa kwa watu 20,000 katika muda wa masaa machache ikiwa ni pamoja na watalii na kusema serikali ilichukuwa hatua thabiti kuhusu suala hilo.

soma pia:Upepo mkali kutatiza shughuli ya kuzima moto Ugiriki

Hata hivyo, ameendelea kusema kuwa wanaweza kufanya bora zaidi bila ya kutoa maelezo zaidi.

Kiongozi huyo pia amesema hali ya hewa itaendelea kutatiza juhudi za kukabiliana na moto huo katika siku chache zijazo.

Awali upinzani ulikuwa umekosoa hali kwamba baada ya siku nane, moto katika visiwa vya Rhodes bado haujadhibitiwa.