1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUgiriki

Upepo mkali kutatiza shughuli ya kuzima moto Ugiriki

Sylvia Mwehozi
23 Julai 2023

Upepo mkali unatarajiwa kutatiza shughuli ya kuzima moto unaowaka katika kisiwa cha Ugiriki cha Rhodes, ambapo takriban watu elfu 30,000 wamelazimika kuhama.

https://p.dw.com/p/4UHVv
Moto, Ugiriki
Watu wakijaribu kuzima moto kwenye kisiwa cha RhodesPicha: Lefteris Diamandis/REUTERS

Upepo mkali unatarajiwa kutatiza shughuli ya kuzima moto unaowaka katika kisiwa cha Ugiriki cha Rhodes, ambapo takriban watu elfu 30,000 wamelazimika kuhama. Kisiwa hicho ni mojawapo ya kivutio kikubwa cha watalii nchini Ugiriki.Ulaya na mataifa mengine yakabiliwa na wimbi la joto kali

Wakati nchi hiyo ikikabiliwa na hali ya joto kali, moto umeendelea kuwaka kwa karibu wiki moja kwenye kisiwa hicho. Mamlaka zimeonya kuwa shughuli ya kukabiliana na miali ya moto, huenda ikachukua siku kadhaa.

Mamlaka ya Zimamoto imetabiri kwamba upepo unatarajiwa kuwa mkali zaidi siku ya Jumapili na hivyo kuzidisha makali ya moto. Moto huo ulifika katika kijiji cha Laerma wakati wa usiku, na kuteketeza nyumba na kanisa, huku hoteli nyingi zikiharibiwa na miale ya moto iliyofika pwani. Watalii wamelazimika kulala, mashuleni na kwenye vituo vya mikutano