1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Chad atangaza kugombea urais

11 Machi 2024

Waziri mkuu aliyeteuliwa na serikali ya Chad, Succes Masra ya Jumapili alisema atashiriki uchaguzi wa rais wa Mei 6, siku nane baada ya aliyekuwa madarakani Mahamat Idriss Deby Itno kutangaza kuwania urais.

https://p.dw.com/p/4dMr8
Paris Treffen Premier Succes Masra Tschad und Premier Gabriel Attal
Waziri Mkuu wa Chad, Succes Masra akiwa na Waziri Mkuu wa Ufarasasa Gabriel Attal Picha: Lafargue Raphael/abaca/picture alliance

 

Kiongozi wa zamani wa upinzani Succes Masra alirejea kutoka uhamishoni na kutia saini mkataba wa maridhiano na Deby Itno kabla ya kuwa waziri mkuu mwaka huu.

Upinzani unasema kuwa uwepo wa mgombea raia ni njama ya kutoa sura ya vyama vingi katika zoezi la upigaji kura lakini kimsingi  kiongozi wa kijeshi ana uhakika kushinda na kwamba wapinzani wake wakuu wamekufa au kukimbilia uhamishoni.

Masra, 40, alifichua azma yake ya kuwania urais katika mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wanaharakati kutoka chama chake cha wapenda mabadiliko, akisema anataka "kuponya mioyo na kuwaunganisha watu".