1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia ametangaza baraza la mawaziri

19 Aprili 2018

Abiy Ahmed aliyeteuliwa mwezi uliopita na muungano unaotawala nchini Ethiopia na Aprili 2 kuapishwa kuwa waziri mkuu ametangaza uteuzi wa baraza hilo katika televisheni ya taifa

https://p.dw.com/p/2wJNA
Äthiopien Neuer Ministerpräsident Abiy Ahmed Ali vereidigt
Picha: picture-alliance/dpa/AP/M. Ayene

Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia Abiy Ahmed ametangaza baraza la mawaziri linalojumuisha waziri wa zamani wa madini ambaye sasa anakuwa waziri wa ulinzi huku pia akiwabakisha mawaziri wa fedha na mambo ya nje waliokuwa katika serikali ya mtangulizi wake. Abiy Ahmed aliyeteuliwa mwezi uliopita na muungano unaotawala nchini Ethiopia na Aprili 2 kuapishwa kuwa waziri mkuu ametangaza uteuzi wa baraza hilo katika televisheni ya taifa.  Waziri Mkuu huyo wa Ethiopia ambaye ni afisa wa zamani wa jeshi ametoa mwito kwa bunge kuidhinisha mabadiliko aliyoyafanya yanayowahusu mawaziri sita pamoja na uteuzi mpya wa mawaziri wengine kumi.  Mawaziri waliosalia waliokuwemo kwenye baraza lililopita ikiwa ni pamoja na waziri wa fedha na mambo ya nje hawakubadilishwa.