1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kishida ataka kukukatana na Kim Jong Un wa Korea kaskazini

Zainab Aziz
25 Machi 2024

Dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini ambaye ni mjumbe wa chama kinachotawala nchini Korea kaskazini amesema waziri mkuu wa Japan, Fumio Kishida ameelezea nia ya kukutana na Kim Jong Un.

https://p.dw.com/p/4e6bd
Fumio Kishida
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida Picha: Kazuhiro Nogi/AFP

Vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini vimeripoti taarifa hiyo.

Waziri Mkuu wa Japan Kishida amesema anataka kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote na anasimamia juhudi za kufanikisha lengo la kufanyika mkutano huo wa kwanza tangu miaka 20 iliyopita. 

Hata hivyo Kim Jong Un amejibu kwa kusema kuboreshwa uhusiano kati ya Japan na Korea Kaskazini kutategemea iwapo Japan itafanya maamuzi ya kisiasa yanayokubalika. Japan iliitawala rasi yote ya Korea kuanzia mwaka 1910  hadi mwaka 1945.