1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wenye silaha wawaua wanajeshi sita wa Nigeria

Lilian Mtono
22 Aprili 2024

Wanajeshi sita wa jeshi la Nigeria wameuawa na watu waliojihami kwa silaha wakati wakifanya doria katika jimbo la kaskazini la Niger siku ya ijumaa.

https://p.dw.com/p/4f3ql
Nigeria -wanajeshi
Wanajeshi wa NigeriaPicha: Sunday Alamba/AP/picture alliance

Wanajeshi sita wa jeshi la Nigeria wameuawa na watu waliojihami kwa silaha wakati wakifanya doria katika jimbo la kaskazini la Niger siku ya ijumaa. Hiki ni kisa cha karibuni zaidi ambapo wanajeshi wanauliwa na magenge ya uhalifu. Wanafunzi 15 watekwa katika kisa cha karibuni zaidi cha utekaji, Nigeria

Msemaji wa jeshi Meja Jenerali Onyema Nwachukwu amesema kwenye taarifa usiku wa Jumapili kwamba wanajeshi hao wa divisheni ya kwanza walikuwa wakifanya doria ya kudhibiti mapigano katika kijiji cha Karaga, kilichopo kwenye eneo la Shiroro, katika jimbo hilo la Niger, wakati waliposhambuliwa.

Eneo hilo kwa kiasi kikubwa limezungukwa na makundi ya wahalifu na mara nyingi huwashambulia wanavijiji pamoja na vikosi vya usalama.

Jeshi la Nigeria pamoja na kupambana na ugaidi katika eneo la kaskazinimashariki, limekuwa likikabiliana na kitisho kinachoibuliwa na magenge hayo yanayowaua wakazi na wanafunzi katika majimbo ya kaskazini na katikati mwa taifa hilo.