1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanne wanasa katika jengo lililoporomoka Nairobi

14 Mei 2024

Timu ya waokoaji imefanikiwa kuwavuta watu wanne waliokuwa wamenasa kwenye kifusi cha jengo moja lililoporomoka katika mtaa wa Mathare ulioko katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

https://p.dw.com/p/4fqaU
Kenia Trümmer
Watu kadhaa wakiwa katika eneo la jengo lililobomolewa huko Mathare Kenya.Picha: DW

Shirika la msalaba mwekundu nchini humo limearifu kwamba bado kuna watu wengine zaidi wanaoshukiwa kunasa kwenye kifusi cha jengo hilo. Watu watatu kati ya wanne waliokolewa wamepelekwa hospitali huku mmoja aliyepata majeraha madogo akitibiwa kwenye tukio. Jengo lililoporomoka lilikuwa katika mchakato wa kubomolewa.Mathare ni mtaa wa makaazi duni uliokumbwa na athari mbaya za mafuriko mwezi huu baada ya mto kujaa maji na kupasua kingo zake kufuatia mvua kubwa zilizonyesha watu chungunzima walipoteza maisha na maelfu kulazimika kuhama makaazi yao.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW