1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Utulivu warudi Mathare

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuN

Utulivu umerudia tena katika mojawapo ya vitongoji duni vikubwa kabisa vya Nairobi hapo jana baada ya siku tano za machafuko kati ya magenge yanayopingana ambapo wakaazi wanasema yameuwa takriban watu wanane.

Kikosi maalum cha polisi kimetumwa katika kitongoji hicho cha Mathare ambapo kina wakaazi 400,000 wa Kenya katika bonde kaskazini mashariki ya Nairobi kuzima machafuko hayo yaliotokana na mzozo juu ya biashara haramu ya pombe ya kieyneji chan’gaaa.

Msemaji wa serikali Alfred Mutua ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kile walichokishuhudia Mathare ni kuibuka kwa uhalifu ulioandaliwa.

Magenge hayo yalipigana kwa kutumia marungu na mapanga na vibandaa kadhaa viliteketezwa na moto.