1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 9 wamekufa baada basi walilokuwamo kushambuliwa India

10 Juni 2024

Watu wenye silaha wamelivamia basi lililokuwa limewabeba mahujaji wa madhehebu ya Kihindu katika eneo la Kashmir lenye kuongozwa na India.

https://p.dw.com/p/4gqp7
India | Shambulio kwenye basi
Mtu aliyejeruhiwa akifikishwa katika Hospitali baada ya basi alilokuwa akisafiria kutumbukia kwenye korongo refu katika eneo la Pouni wilayani Reasi ya Jammu, India, Jumapili, Juni 9, 2024.Picha: Channi Anand/AP Photo/picture alliance

Na kufanya litumbukie kwenye bonde na hivyo kusababisha vifo vya takriban watu tisa na wengine 23 kujeruhiwa.

Shambulio hilo lilitokea makadirio ya kiasi cha muda wa saa moja kabla ya Waziri Mkuu wa madhehebu ya Kihindu Narendra Modi kuapishwa kwa muhula wa tatu Jumapili jioni katika mji mkuu New Delhi.

Vyanzo kutoka katika jeshi la polisi vimesema taarifa za awali zinaonesha washambuliaji walikuwa katika eneo la tukio wakilisubiri basi hilo na baada ya kulishambulia dereva alishindwa kulidhibiti na hivyo kutumbukia bondeni.

Kashmir ambayo imegawanywa kati ya India na Pakistan tangu uhuru wao mwaka 1947, na pande zote mbili zinadai mamalaka ya kujitawala.