1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUhispania

Watu 7 mbaroni kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya Vinicius Junior

Bruce Amani
24 Mei 2023

Watu saba wakamatwa kuhusiana na ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa soka Vinicius Junior.

https://p.dw.com/p/4Rjy6
Brasilianischer Fußball-Spieler Vinicius Junior
Picha: Alberto Saiz/AP/picture alliance/dpa

Polisi nchini Uhispania imewakamata watu wanne wanaotuhumiwa kutundika kwenye daraja sanamu la mchezaji nyota wa kandanda mweusi.

Watuhumiwa hao walitumia sanamu nyeusi ya puto ikiwa na jezi nambari 20 ya Vinicius Junior na kufunga kamba kwenye shingo.

Waliitundika kwenye daraja karibu na uwanja wa mazoezi wa Real Madrid asubuhi ya mechi ya watani wa jiji dhidi ya Atletico Madrid.

Iliambatana na bango lililokuwa na ujumbe wa: Madrid inaichukia Real.

Real Madrid ilisema ubaguzi aliofanyiwa mshambuliaji wake wa Kibrazil Vini Junior wakati wa mechi ya mwishoni mwa wiki ulifikia kuwa uhalifu wa chuki.

Mnamo Jumanne, polisi iliwakamata watu watatu mjini Valencia kuhusiana na matusi hayo.

Ligi ya Uhispania ilikuwa imewasilisha malalamiko ya matukio tisa ya uhalifu wa ubaguzi wa rangi dhidi ya Vinicius katika misimu miwili iliyopita.