1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

6 wauwawa katika makabiliano kambi ya wakimbizi Bangladesh

7 Julai 2023

Watu sita wameuwawa katika kambi ya wakimbizi huko Bangladesh kufuatia vurugu zilizozuka masaa machache baada ya ziara ya kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, kukusanya ushahidi.

https://p.dw.com/p/4TZ9M
Rohingya Flüchtlingslager in Bangladesch
Picha: Emre Ayvaz/AA/picture alliance

Faruq Ahmed, ambaye ni msemaji wa kikosi kinachohusika na usalama katika kambi za wakimbizi, ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP, kwamba, watu watano waliuwawa kwa kupigwa risasi katika makabiliano yaliyotokea kabla alfajiri ya leo.

Machafuko hayo ya wiki hii ndiyo ya hivi karibuni kutokea katika msururu wa mapambano makali kati ya makundi mawili hasimu yaliyo katika kambi hizo za wakimbizi. Bangladesh ni makao ya karibu watu milioni moja wa jamii ya Rohingya, ambao idadi kubwa walikimbia kamatakamata iliyofanywa na jeshi la Myanmar.

Operesheni hiyo ya jeshi la Myanmar sasa inachunguzwa na mahakama ya ICC kubaini iwapo itakidhi kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya halaiki.