Watu 30 wafamaji Uganda | Matukio ya Afrika | DW | 27.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Watu 30 wafamaji Uganda

Karibu watu 30 wamekufa maji baada ya boti ya abiria iliyokuwa imejaa kupitiliza kiasi kuzama katika Ziwa Albert, magharibi mwa Uganda.

Polisi wa Uganda wameripoti kuwa boti hiyo ilikuwa imewabeba watu 45. Wameongeza kuwa watu 21 hawajulikani walipo, wakati miili tisa ikiokolewa. Wengine 15 waliokolewa na wavuvi pamoja na polisi. Ajali za majini ni jambo la kawaida nchini Uganda, kwa sababu vyombo vingi vya majini vimekuwa vikitengenezwa ndani bila ya kuwapo na vifaa vya uokoaji.