1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Watu 2,000 wapoteza maisha mjini Derna kufuatia mafuriko

12 Septemba 2023

Vikosi vya uokoaji mashariki mwa Libya vimepata miili ya mamia ya watu kutoka kwenye vifusi katika mji wa pwani wa Derna uliokumbwa na mafuriko makubwa.

https://p.dw.com/p/4WF5K
Mji wa Mashariki mwa Libya Derna ukiwa umeharibikwa kwa mafuriko
Mji wa Mashariki mwa Libya Derna ukiwa umeharibikwa kwa mafurikoPicha: AA/picture alliance

Mamlaka nchini humo imeeleza kuwa, inakadiriwa kuwa watu 2,000 wanaaminika kupoteza maisha katika mji wa Derna.

Kimbunga cha Daniel kimesababisha mafuriko makubwa katika maeneo mengi ya mashariki mwa Libya, lakini uharibifu mkubwa umetokea katika mji wa Derna ambapo mvua na mafuriko yamevunja mabwawa na kusomba vijiji.

Soma pia:Kimbunga Daniel chaua watu zaidi ya 2,000 Libya

Waziri Mkuu wa serikali upande wa mashariki ya Libya Ossama Hamad amesema maelfu ya watu hawajulikani waliko na kwamba wengi wao wanaaminika kusombwa na maji.

Shirika la hilali nyekundu la Libya limesema leo kuwa, timu yao imehesabu zaidi ya watu 300 waliokufa mjini Derna. Serikali ya Mashariki mwa Libya imeutangaza mji huo wa Derna kama eneo la maafa.