1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watu 200 watekwa nyara na magaidi kaskazini mwa Nigeria.

7 Machi 2024

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Nigeria, imesema watu 200 wengi wao wanawake na watoto waliopoteza makaazi yao kufuatia ghasia kaskazini mashariki mwa Nigeria, wametekwa nyara na kundi la Boko Haram.

https://p.dw.com/p/4dH1I
Maiduguri ndio mji mkuu wa Jimbo la Borno
Wanamgambo wa Boko Haram wanaendesha harakati zao kaskazini mwa NigeriaPicha: Florian Gaertner/photothek/IMAGO

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Nigeria, imesema watu 200 wengi wao wanawake na watoto waliopoteza makaazi yao kufuatia ghasia kaskazini mashariki mwa Nigeria, wametekwa nyara na kundi la Boko Haramwalipokuwa wanatafuta kuni karibu na mpaka wa Chad.

Waathiriwa hao walikuwa wamezunguka katika kambi kadhaa wakitafuta kuni katika jimbo la Borno, wakati walipovamiwa na kutekwa. Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria, Mohammed Fall, amesema iIdadi kamili ya watu waliotekwa hadi sasa bado haijajulikana lakini inakadiriwa kufika 200.

Kisa hicho kinasemekana kutokea siku kadhaa zilizopita lakini taarifa zake zimetolewa leo kufuatia kudhibitiwa kwa mawasiliano katika eneo la Gamboru.

Fall amesema licha ya kutolewa taarifa ya kuachiwa kwa kinamama wazee na watoto walio chini ya miaka 10, bado kuna idadi kubwa ya watu hawajulikani waliko.