1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 13 wauawa kwenye mapigano na wanamgambo Iran

Josephat Charo
4 Aprili 2024

Watu wapatao 13 wameuawa baada ya mapigano makali kuzuka kati ya vikosi vya usalama na wanamgambo kusini mashariki mwa Iran.

https://p.dw.com/p/4ePxm
Iran Baluchistan-Sistan
Wakaazi wa mkoa wa Sistan-Baluchistan kusini mashariki mwa Iran wakiandamana.Picha: UGC/AFP

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran, Majid Mirahmadi, alisema siku ya Alkhamis (Aprili 4) kwamba wanamgambo walifanya shambulizi kubwa kwenye kambi za Kikosi cha Walinzi wa Mapiinduzi kusini mashariki mwa taifa hilo.

Washambuliaji wanane na maafisa watano wa vikosi vya usalama waliuliwa kwenye makabiliano yaliyotokea.

Soma zaidi: Raisi: Iran italipa kisasi shambulio la ubalozi wetu Syria

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali (IRNA), mashambulizi hayo yalitokea mapema alfajiri ya Alkhamis kwenye kambi za kijeshi katika miji ya Rask na Chahbahar katika jimbo la Sistan-Baluchistan.

Kundi la wanamgambo la Jaish al-Adl linalopigania uhuru wa eneo la kusini mashariki mwa Iran lilidai kuhusika na shambulizi hilo.